Kamati ya fedha na utawala ya Manispaa ya Kigamboni ikiongozwa na Mstahiki Meya Mhe.Maabad Suleiman Hojja wamefanya ziara ya kutembelea ujenzi wa ofisi unaoendelea katika eneo la Gezaulole kata ya Somangila ambapo walijionea hatua iliyofikiwa na mkandarasi ambaye ni wakala wa ujenzi TBA.
Meya Maabad aliwahimiza wakandarasi kuongeza kasi ili kumaliza hiyo kazi kwa wakati kwani watumishi wa Halamashauri wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kuwa katika ofisi zilizopo mbali mbali jambo ambalo ni kero hata kwa wananchi wanaofika kupata huduma kwani inawalazimu kusafiri kutoka ofisi moja kwenda nyingine.
Mkandarasi huyo aliwahakikishia kamati kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi ndani ya muda waliopanga ambapo wanatajia kukamiliza ujenzi ifikapo mwezi Septemba mwaka huu wa 2018.
Mhandisi msimamizi wa mradi huo dg Edwin Godfrey alisema mpaka sasa wapo kwenye hatua ya msingi na wapo ndani ya muda waliojipangia hivyo wanatarajia watakamilisha kazi hiyo kwa wakati na hivyo kuwawezesha watumishi wahalmashauri kuhamia ifikapo Octoba 2018.
Ujenzi huo unagharamiwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Serikali kuu unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 5.1 mpaka kukamilika kwake.
Hatua za awali za ujenzi wa jengo la utawala
Kamati ya fedha na utawala walipotembelela mradi wa jengo la utawala la Manispaa ya Kigamboni
ukaguzi wa mradi ukiendelea
ramani zinazoonesha jengo litakavyokuwa mara baada ya kukamilika
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa