Habari picha ikimuonyesha Mwenyekiti wa Kamati ya fedha na utawala na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe Ernest Mafimbo akiongoza ziara ya kamati yake yenye lengo la kutembelea na kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kipindi cha robo ya 4 ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Katika ziara hiyo Mhe Mafimbo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti tofauti.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Mjimwema Diwani wa Kata ya Mjimwema Mhe. Omary Ngurangwa amesema kukamilika kwa Kituo hicho kutasaidia kusogeza huduma ya Afya kwa wakazi wa Kata yake ambao hulazimika kuifuata huduma hiyo katika Kata ya Vijibweni au Kigamboni.
Aidha kamati ilifanikiwa kutembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Vumilia ukooni iliyopo kata ya Kisarawe ii, ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Mjimwema kilichopo kata ya Mjimwema pamoja na ujenzi wa jengobla mama na Mtoto katika Hospitali ya Vijibweni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa