Kamati ya Fedha na Utawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ikiongozwa na Mstahiki Meya Mh.Maabad Hojja ,imefanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Manispaa katika kata za Somangila,Kimbiji, Kisarawe II na Vijibweni.
Moja ya miradi mikubwa iliyotembelewa na kamati hiyo ni ujenzi wa ofisi ya Manispaa inayojengwa katika eneo la Gezaulole kata ya Somangila na Mkandarasi wake akiwa wakala wa Ujenzi wa serikali (TBA) ambapo thamani ya mradi huo ni shilingi Bilioni tano ambapo mpaka sasa mkandarasi yupo katika hatua za awali za usafishaji wa eneo, upimaji wa udongo pamoja na ujenzi wa barabara za kufika eneo la mradi. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu 2018
Mradi mwingine uliotembelewa ni ujenzi wa barabara kata ya Kimbiji kwa kiwango cha changarawe, mradi wa maji Kimbiji pamoja na ujenzi wa chumba cha X-ray katika hospitali ya vijibweni.
Katika majumuhisho ya ziara hiyo, wajumbe wa kamati wamepongeza hatua zilizofikiwa pamoja na kueleza changamoto walizoziona katika baadhi ya miradi.
Diwani wa kata ya Kibada ambaye pia ni Naibu Meya amesema muda uliobaki kukamilisha ujenzi katika hospitali ya Vijiweni ni wiki tatu huku kazi iliyobaki ikionekana kuwa kubwa, hivyo amemtaka mhandisi wa Manispaa Eng. Pius Mutechura kusimamia ujenzi huo ukamilike kwa wakati lakini pia ubora wake uzingatiwe.
Akifunga kikao cha majumuisho hayo, Mstahiki Meya amewataka watendaji kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati lakini pia thamni ya fedha inayotumika ilingane na miradi husika.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa