Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepongeza maendeleo ya Ujenzi Wa miradi ya maendeleo hususani sekta ya Afya.
Pongezi hizo zilitolewa leo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya majukumu yao.
Kamati ya Fedha ilisema imeridhishwa na hatua za ujenzi miradi ya maendeleo hususani vituo Vya Afya na kuwapongeza wanakamati na wataalamu wanaofanikisha ukamilikaji wa majengo hayo.
Aidha wametaka ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri kuongezwa kasi ya ujenzi ili watumishi waweze kuhamia Kwa wakati uliopangwa na kufanya Kazi kwenye Mazingira mazuri.
Kamati ya Fedha ilitembelea miradi mitano, mradi Wa ujenzi wa kituo cha Afya Kimbiji, bwalo la wanafunzi Shule ya Sekondari Nguva, eneo la ujenzi Wa Hospitali ya Wilaya ,ujenzi wa jengo la Utawala na kituo cha Afya Kigamboni.
wanakamati wakikagua chumba cha upasuaji kwenye kituo cha afya kimbiji
wajumbe wa kamati wakisalimia wagonjwa waliokuwa wakisubiri majibu yao ya vipimo kwenye maabara mpya ya kituo cha Afya Kimbiji.
muonekano wa chumba cha upasuaji kwenye Kituo cha Afya Kimbiji
Jengo la kuhifadhia maiti lililopo kwenye kituo cha Afya kimbiji ambalo awali halikuwepo.
wajumbe wa kamati ya Fedha wakitoa maelekezo machache walipotembelea eneo la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
Wajumbe wa kamati ya fedha wakipata maelezo kutoka kwa mhandisi wa Manispaa aliyeshika karatasi walipotembelea eneo la ujenzi wa hospitali ya Wilaya.
Wajumbe wa kamati ya fedha walipotembelea ujenzi wa Bwalo la wanafunzi Nguva Sekondari.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Bwalo Shule ya Sekondari Nguva
ukaguzi wa ujenzi wajengo la Utawala
jengo la utawala kwa muonekano wa sasa katika hatua ya ujenzi
viongozi wakifurahia ujenzi wa kituo cha afya Kigamboni, walipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo
mhandisi wa Manispaa Bw.Pius Mtechura akiongoza wajumbe kueleka kwenye jengo lingine linalojengwa ndani ya Kituo cha Afya Kigamboni
jengo la kuhifadhia maiti linalojengwa kwenye kituo cha afya kigamboni.
muonekano wa ndani eneo la kusafishia
wajumbe wakikagua miundombinu ya eneo la kusafishia mwili kwenye jengo la kuhifadhia maiti.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa