Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kigamboni imefanya uchaguzi wa viongozi wa jukwaa la huduma ndogo za kifedha watakao kuwa na jukumu la kusimamia na kuhamasisha vikundi vya huduma za kifedha kusajiliwa sambamba na kutoa elimu ya ujasiliamali.
Akizungumza wakati wa uchaguzi huo Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii Bi Sigilinda Mdemu alisema wao kama Halmashauri wanajukumu la kuwaunganisha na sekta za kifedha ikiwemo mabenki ili kupatiwa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha kuendeleza na kukuuza vikundi vyao.
Aidha Bi mdemu alitoa elimu ya namna ya kuendesha vikundi vya huduma ndogo za kifedha huku akiwaelekeza namna ya kujiinua kiuchumi kwa kuanzisha viwanda vidogo vya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika majumbani ikiwemo za usafi pamoja na bidhaa za chakula.
Sambamba na utoaji wa elimu bi Sigilinda amesisitiza walimu wa vikundi kujisajili na kuhamasisha vikundi wanavyovifundisha kusajiliwa kwenye mfumo
‘Serikali ina lengo zuri na wananchi wake hivyo sisi kama wanufaika tutekeleze yale yote ambayo wataalam wa idara ya maendeleo wanatuelekeza ili kuipa wepesi Serikali yetu kututekelezea yale waliyoyaadhimia kwa wananchi wake’. Alimalizia bi Mdemu.i
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa