Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma almasi Nyangassa ameitaka jamii kutambua kuwa jukumu la ulinzi kwa watoto ni letu sote na hivyo ni vyema kuungana pamoja kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya St.Joseph iliyopo kata ya Kibada Mhe.Fatma amesema kuwa mtoto anapaswa kulindwa bila kujali jinsia kwani malezi yameonesha watoto wa kike ndio waliopewa kipaumbele na wakiume kusahaulika .
Aidha amewataka walimu,wazazi na walezi kuhakikisha wanatoa taarifa za kikatili zinazohusu watoto na kuacha tabia za kuwaficha wahalifu kwani kwa kufanya hivyo kunapelekea Serikali kushindwa kuchukua hatua na kumyima mtoto haki yake ya kisheria.
"Mtindo wa maisha umebadilika wazazi wamekuwa watafutaji na walimu wamekua na muda mwingi na watoto, naomba walimu tulindieni watoto hawa, nawewe mzazi hatakama mda mwingi unautumia kwenye kazi haizuii jukumu lako kama mzazi kuwa karibu na mtoto wako, jenga tabia ya kumsikiliza na kumsaidia anapohitaji msaada" Alisema
Mhe.Fatma.Ameongeza kwa kusema kuwa Serikali inamuangalia mtoto kwa jicho la mbali na ndiomaana kumekuwa na harakati za kumlinda hivyo jamii iungane katika jitihada hizo ili Taifa litengeneze watoto wanaojielewa na viongozi bora wa hapo baadae.
Mhe Fatma pia amewataka watoto kuhakikisha wanakua wa kwanza kujilinda kwa kutoa taarifa kwa wazazi, walezi na waalimu pindi wanapoona dalili za kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kupokea vitu/zawadi kwa watu wasiowajua.
Kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bi.Happy Luteganya amesema kuwa kumekuwa na harakati nyingi za kumkomboa mtoto dhidi ya ukatili hivyo ameiomba jamii kuungana na Serikali chini ya Waziri Dorooth Gwajima ili kufikia azma ya kutokomeza kabisa.
Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Mjimwema na mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Mhe. omary Ngurangwa amesisitiza watoto kujitambua,kujilinda na kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya kikatili kwani Taifa hili linawategema sana.
Maadhimisho haya yalijumuisha michezo mbalimbali na maigizo pamoja na utoaji vyeti kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangassa akizungumza na wazazi, walezi na watoto kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwenye viwanja vya shule ya Msingi St.Joseph.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangassa akifurahi pamoja na watoto akiwa ameambatana na viongozi wengine.
Watoto Shule ya Msingi Kibada wakipita kwa maandamano.
Kaimu Mkurugenzi Bi.Happy Luteganya akizungumza na walezi kuungana mkono jitihada za Serikali kutokomeza ukatili.
Wimbo wa umuhimu wa kulinda mtoto wa kiume ukifanywa na wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mizimbini.
Watoto wa shule ya msingi Mizimbini wakicheza mchezo wa kuvuta kamba
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii na Diwani wa Kata ya Mjimwema Mhe.Omary Ngurangwa na watoto
Watoto wakitoa ujumbe kwa njia ya bango
Watoto wakiigiza igizo la umuhimu wa Shule
Mkuu wa Wilaya Mhe.Fatma Nyangassa akipanda mti kama kumbukumbu ya maadhimisho.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi St.Joseph wakiwa kwenye onesho la ngoma
Kiongozi wa Shule ya Msingi St.Joseph Sister Teresia akipanda mti kama kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa