“Natoa wito kwa Jamii kuendelea kutoa huduma ya kwanza kwa watu wenye dalili za ugunjwa wa Corona, nasi pia kama Serikali tumejipanga. Hata wakija Watalii tupo tayari kutoa huduma”
Ni wito uliotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Sarah Msafiri wakati akipokea msaada wa vifaa tiba uliotolewa na Shirika la usafirishaji wa mafuta kati ya Tanzania na Zambia (TAZAMA PIPELINE) na hatimaye kuukabidhi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu, Ng’wilabuzu Ludigija kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na janga la Corona.
Aidha katika mabidhiano hayo vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milion 35 vilitolewa ikiwemo, Ndoo za kunawia Mikono (Vitiririshi), Vifaa vya kupimia joto la mwili, Barakoa /Mask pamoja na Glovu (Gloves) na vimewasilishwa na Meneja Mkuu wa Shirika hilo Ndugu, Abraham Saunyama.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa