"Serikali ya awamu ya sita ya mama Samia Suluhu Hassan iko mbele katika kuhakikisha inasimamia haki wajibu na maendeleo ya Mtoto."
Kauli hiyo imetolewa leo na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi. Dalmia Mikaya (Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni) katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kiwilaya katika Uwanja wa Mjimwema.
Katika maadhimisho hayo Bi Dalmia ameitaka jamii kukaa karibu na watoto ili waweze kupata haki zao za msingi na kuwajenga kiakili na kiroho
Aidha amewaasa watoto kujiepusha na mambo mabaya yanayopelekea kuaribika kwa maadili na kupata mimba za utotoni
Akimuwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa Aron Bullu (Mkuu wa idara ya Mifugo na Uvuvi) ameeleza kuwa Manispaa imezipokea changamoto zote zilizotolewa na watoto katika risala yao na watahakikisha wanazifanyia kazi na kuzitatua.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhumishwa tarehe 16/5 kila mwaka ikiwa ni kama kumbukumbu ya watoto waliokufa wakitetea haki zao huko Soweto South Africa mwaka 1976
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa