Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe Fatma Almasi Nyangasa amewataka walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuvienzi na kutunza Samani mbalimbali zinazotolewa na wadau ikiwa ni njia ya kuheshimu michango hiyo katika secta mbalimbali.
Mhe Nyangasa ametoa wito huo mchana wa leo alipokuwa akipokea msaada wa viti pamoja na meza zake 200 vilivyotolewa na shirika la Bima (NIC) vyenye thamani ya shilingi Mil 20 Katika hafla fupi iliyofanyika shule ya Sekondari Abdul Jumbe iliyopo Manispaa ya Kigamboni.
Katika makabidhiano hayo pia Mhe Mkuu wa wilaya amesema Serikali inatambua mchango wa vijana katika kukuza maendeleo ya nchi kupitia nyadhifa mbalimbali na misingi ya uongozi bora huanza katika ngazi ya chini kwa kutatua changamoto katika secta ya elimu.
Akitoa msaada huo mwakilishi wa Meneja wa shirika la Bima Ndugu Karimu meshack ambaye ni Meneja Uhusiano katika shirika hilo amesema, Shirika limetoa msaada huo ikiwa ni kutambua juhudi za Serikali katika kuboresha secta ya elimu kupitia sera ya elimu bila malipo ambapo uhitaji wa viti na meza umekuwa ni changamoto kubwa kutokana na muitikio mkubwa wa jamii.
Aidha amaeahidi kuendelea kushirikiana na Wilaya ya Kigamboni katika kutatua changamoto mbalimbali hususani katika secta ya elimu.
Akiongea kwa niaba ya Wanafunzi wa Abdul Jumbe mwanafunzi Lusajo Mwasilu amelipongeza Shirika kwa kuwapatia nyenzo zitakazowasaidia katika masomo yao na wameahidi kufanya vizuri katika masomo yao kupitia msaada huo.
Shirika la Bima limetoa juma ya viti na meza 200 vilivyogawanywa katika shule 3 ambazo ni shule ya Sekondari Abdul Jumbe viti na meza 100, Kisarawe II viti na meza 50, pamoja na Minazini Viti na meza 50
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa