Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi (MB) Mhe. Selemani Jafo amewapongeza Vijana Baraka Erasto na Aboubakari Ali Aboubakari wamiliki wa chuo cha afya cha Kigamboni Healthy City Colledge kwa uzalenzo , ukomavu na kuwa mfano kwa Vijana wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuamua kutumia elimu waliyoipata kwa kujenga chuo kinachohudumia wanafunzi 1700.
Waziri ameyazungumza hayo leo alipokuwa kwenye uwekeji wa jiwe la msingi wa Kituo cha Afya kinachojengwa na chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kusogeza huduma kwa wakazi wa Tarafa ya Somangila.
Mhe. Jafo amesema kuwa amefurahishwa sana na namna vijana hao walivyoamua kujiwekeza na kwamba watakuwa ni Vijana wa kupewa kipaumbele na Serikali kwa namna ambavyo wameamua kuunga mkono Juhudi za Rais Dk.John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda.
“Hospitali hiii mnayojenga itawasaidia wananchi wa maeneo haya kupata huduma lakini pia kuongeza maarifa kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosoma hapa, upatikanaji wa ajira hivyo hongereni sana na nasema kutoka moyoni nimefarijika” Alisema Mhe. Jafo
Aliongeza kuwa ushirikiano ambao wameingia na nchi ya Poland katika kutekeleza malengo yao ni mzuri na usiwe kwaajili ya kujenga kiwanda cha madawa pekee bali iwe hata kwa vifaaa vingine vya Kitabibu vinavyohitajika na kuwasisitiza pia kuwa makini namikataba ya kisheria ambayo wanaingia ili wasije wakapoteza umuliki wao wa kihalali.
Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi yake itatoa cheti cha heshima kwa kuwatambua Vijana hao kwa kazi kubwa waliyoifanya kwasababu wamekuwa ni sehemu ya kuongeza ufanisi wa kazi za Ofisi ya Rais Tamisemi na kwamba wamefanya jambo kubwa kwenye Taifa la Tanzania.
Aidha waziri amewaagiza Mkurugenzi na Katibu tawala wa Wilaya kuwasaidia vijana hao kwa lolote wanatalolihitaji kwenye utekelezaji wa mipango yao ili kuwaunga mkono hususani kwenye suala la Ardhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo hicho Bw. Amesema kuwa ujenzi wa Hospitali hiyo umeanza aprili 2019 na kutarajiwa kumalizika Desemba 2019 na baada ya ukamilifu itajulikana kama Kigamboni City Colledge teaching Hospital, ambapo utagharimu kiasi cha Bilioni 2.
Hospitali hiyo itakua na majengo 2 ya wodi ya wazazi,vyumba viwili vya upasuaji,chumba 1 cha wagonjwa wa dharula, maabara ya kisasa itakayokuwan na City scan na MRI na chumba cha kuhifadhia maiti.
Aidha Chuo hicho kinampango wa kujenga kiwanda cha madawa chenye uwezo wa kuzalisha vidonge Bilioni 3, chupa za sirapu Milioni 400,chupa za infusion Milioni 300 kwa mwaka ifikapo Octoba 2022 ili kuendana na kauli ya Rais kwa kuwa na Tanzania yenye Viwanada, kuzalisha wataalamu na ajira ambapo kiwanda hicho kinatarajiwa kugharimu kiasi cha Bilioni 10.
Wakati huohuo Mhe. Selemani Jafo amewapongeza Viongozi wa Wilaya ya Kigamboni kwa kazi nzuri wanazofanya na kwamba Wilaya ya Kigamboni ianenda vizuri na anafarijika sana na utendaji wa kazi .
Waziri amesema kuwa Kigamboni ni Wilaya Mpya na katika Wilaya zilizoanzishwa Kigamboni inaenda vizuri na kwamba miradi ya maendeleo inayotekelezwa inatekelezwa vyema na anamini hata miradi inayotarajiwa kutekelezwa itafanyika vyema pia.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa