Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Enedy Mwanakatwe leo tarehe 30/9/2024 amefungua mafunzo ya utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya wilaya na kata Yenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao katika maeneo ya mikakati, miongozo na kanuni juu ya utoaji na usimamizi wa mikopo.
Akizungumza wakati wa Mafunzo Bi Enedy alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameirudisha mikopo ili wananchi waweze kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo hiyo yenye masharti nafuu isiyo na riba.
Akiendelea amesema maafisa maendeleo wanajukumu la kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuachana na mikopo ya kausha damu yenye kudhalilisha utu wa mtu na badala yake wananchi kupitia maafisa maendeleo ya jamii wahamasishwe utaratibu wote wa kuweza kuunda vikundi na kuomba mikopo kwa kuzingatia nyaraka zote zitakazo wawezesha kupata mikopo itakayowawezesha kuboresha uchumi wa familia na jamii kwa ujumla
Amesema tayari utaratibu wa awali umeanza kwa utolewaji wa mikopo hiyo umeshaanzishwa kwa kuwapa wataalamu ngazi ya Halmashauri na kata kwa kuwapatia mafunzo hayo
Pamoja na mambo mengine Bi Enedy aliwataka maafisa maendeleo kuendelea kutumia nafasi yao ya kusimamia jamii kwa kuhamasisha kujianda kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura zoezi litakalo anza tarehe 11 hadi 20 mwezi octoba.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa