Ikiwa ni mwendelezo wa habari za uboreshaji wa huduma za afya, Kituo cha afya Kigamboni kilipokea pia fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha shilingi milioni 400 za utanuzi wa majengo ya kutolea huduma.
Ujenzi wa majengo mapya ya upanuzi wa kituo hicho ulianza tarehe 20/9/2018 ambapo ilijumuisha majengo ya maabara, upasuaji,jengo la wazazi na chumba cha kuhifadhia maiti.
Ujenzi wa majengo haya umetumia mfumo wa force account ( Mfumo wa kutumia mafundi wa kawaida wanaopatikana eneo husika badala ya wakandarasi na vifaa vya ujenzi vinanunuliwa kwa bei ya sokoni sio ya zabuni) wanachi walihusishwa moja kwa moja kwa kutumia kamati walizoziunda wenyewe za kusimamia ujenzi na kuhakikisha taratibu za manunuzi zinafuatwa kwa kusimamiwa na wataalamu wa manispaa.
Hadi sasa ujenzi upo kwa 96% ambapo jengo la maabara lipo kwenye hatua ya MSINGI.
Awali Kituo cha Afya kigamboni hakikuwa na jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti, hivyo uwepo wa majengo hayo utaboresha huduma za afya .
jengo pacha linalojumuisha eneo la upasuaji na eneo la mama na mtoto.
muonekano wa mbele
muonekano wa ndani jengo la upasuaji na mama
jengo la kuhifadhia maiti ambalo awali halikuwepo
wataalamu wa manispaa na klamati ya fedha walipotembelea na kufanya ukaguzi kwenye eneo la kuoshea miili.
sehemu ya kuoshea mwili hatua iliyofikiwa.
viongozi wakifurahia mandhari ya ujenzi wa jengo pacha linalojumuisha upasuaji na mama na mtoo
jengo la maabara likiwa katika hatua ya msingi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa