katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg.Aboubakar Kunenge amepongeza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kuonesha vitu mbalimbali ambavyo hakutegemea kuviona kwenye maonesho ya wakulima nane nane ikizingatiwa Halmashauri bado changa.
"Nyie najua ni wapya, sikutegemea kukuta vitu vikubwa namna hii katika banda lenu, kwakweli nawapongeza sana na mwakani mfanye vizuri zaidi" alisema Katibu Tawala.
Katibu tawala amewataka wataalamu kutumia taaluma zao katika kuwahudumia wananchi kwani wapo kwenye uhitaji wa mawazo kutoka kwa wataalamu, ni vyema wakajipangia mikakati ya kuwafikia kila wakulima na wajasiliamaliili kukuza uchumi wa viwanda.
Kwenye maonesho ya wakulima nanenane Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imewweza kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa kibiashara na wananchi wa Kigamboni ikiwemo Kilimo cha mazao mbalimbali, ufugaji wa mifugo kwa njia ya asilia na kisasa pamoja na ufugaji wa samaki wa kisasa aina ya Sato na Kambale.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inawakaribisha wananchi na wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta za kilimo, mifugo na viwanda kwani inamaeneo ya kutosha ambayo bado hayajaendelezwa.
kilimo cha viriba kinachotoa fursa kulimwa hata kwenye eneo dogo hususan nyumbani
mazao mbalimbali yanayostawi kwenye ardhi ya Kigamboni
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam Ndg.Aboubakar Kunenge akitembelea kuona shughuli za kilimo zinazofanywa na Manispaa ya Kigamboni.
zao la mpunga
zao la pilipili
Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam akipata elimu ya ufugaji wa kisasa alipotembelea kuona bwawa la ufugaji wa samaki aina ya sato wanaofugwa kisasa kwenye banda la maonesho ya wakulima nanenane
Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Ndg.Aboubakar Kunenge akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wajasiliamali wa Kigamboni
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw.Charles Mkombachepa akitoa elimu ya afya na kueleza namna mifugo wanavyoweza kuathiri afya za wafugaji kwa Katibu Tawala wa Mkoa alipotembela banda la afya kwenye maonesho ya wakulima nanenane
Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo Bw.Karume Chausa akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Tawala Mkoa alipotembelea kuona baadhi ya mazao yanayopatikana ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa