Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigamboni leo kwa pamoja limepitisha taarifa ya hesabu za mwisho yaani Final Accounts zilizoishia 30.06.2021 ikiwani takwa la kisheria na kuwapongeza watendaji kwa kukamilisha taarifa hiyo ikiwa ni mwaka wa tano kwa Halmashauri kufunga hesabu zake tangu kuanzishwa na kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo.
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Fedha Jenoveva Meshi amesema kwa mwaka huu wa fedha 202/2021 imefunga vitabu vitano vya hesabu za mwisho ambavyo ni, Kitabu kikuu (consolidated financial statements), Mfuko wa afya ya pamoja (Health Basket financial statements 202/2021), Mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye wenye ulemavu (women, youth and disability financial statement), mradi wa tofali (Bricks projects financial statement), na Mfuko wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF project financial statement).
Aidha katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe.Dotto Msawa ameshauri kuepuka baki ya fedha kwa fedha zinazoletwa na serikali kuu waajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Charles Lawisso amesema kuwa amepokea mapendekezo yote yaliyotolewa ikiwa na kujitahidi kutumia fedha kadri zinavyoletwa ingawa wakati mwingine inakua ngumu kutokana na sheria za manunuzi na fedha hizo kutofika kwa wakati.
Taarifa za uwasilishwaji wa hesabu za mwisho zimefanyika leo kwenye kikao cha Baraza maalumu lililofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni mhe. Ernest Mafimbo katikati akizungumza wakati wa kikao cha Baraza, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Charles Lawisso na kulia ni Naibu Meya Mhe. Stephano waryoba.
Jenoveva Meshi mhasibu wa Manispaa akisoma taarifa ya kufunga hesabu za mwaka kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara.
Kaimu Mkurugenzi Charles Lawisso akipokea ushauri na maelekezo kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani wakati wa kikao.
Diwani wa Kata ya Vijibweni na Kata ya Kibada wakifatilia kwa makini uwasiliswahji wa taarifa ya hesabu.
Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe. Dotto msawa akitoa ushauri wa kutumia feda vizuri na kuepuka baki.
baadhi ya Wataalamu wa Manispaa walioshiriki kikao hicho.
waheshimiwa Madiwani wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya Hesabu.
wataamu wa Manispaa wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa Taarifa za Hesabu.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa