leo eneo hili litakua chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Hayo yamesemwa leo Mei 17,2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe . Albert Chalamila alipowasili kwenye eneo lenye mgogoro wa ardhi lililopo mtaa wa Muhimbili kata ya Pembamnazi wilaya ya Kigamboni.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amefanikiwa kurejesha hekari 200 zilizokua zinamilikiwa na wamiliki 6 ambao walijitwalia eneo hilo kwa njia za udanganyifu ikiwemo kughushi nyaraka za umiliki na mauziano.
Akitoa maagizo kwa kamishina wa ardhi Mkoa wa Dar es salaam Shukrani kyando Mhe Chalamila alisema...
" nikuombe kuharakisha upimaji wa eneo hili na kuuza viwanja kwa wananchi wenye uhitaji huku akisisitiza kutengwa kwa maeneo ya huduma za jamii ikiwemo shule na kituo cha afya".
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa viongozi ngazi ya kata kuwa mstari wa mbele kusimamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbali mbali huku akiwataka kulinda haki ya umiliki wa ardhi kwa kila mwananchi huku akiwaonya kuacha kushiriki katika udanganyifu wa kuuza maeneo
Hata hivyo Kamishina wa ardhi mkoa wa Dar es salaam alipata wasaa wa kutoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa muhimbili wa kulipa pango la ardhi huku akiwasisitiza kulipa kodi zao kabla ya tarehe 1/7/2024.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa