Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Sara Msafiri Ally amepokea misaada ya mashuka na Matenki ya maji kutoka kampuni ya mawasiliano Halotel
Misaada hiyo yenye thamani ya shilingi milioni tano ni Mashuka 100 na matenki 10 yenye ujazo wa lita 5000 kila mmoja.
Meneja wa Biashara wa kampuni hiyo Ndg NguyenTien Ding amesema misaada hiyo ni sehemu ya kampuni yao kurudisha faida kwa wananchi ambao ndio wateja wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija amesema misaada hiyo imekuja kwa wakati kwani katika Halmashauri yake kuna vituo vya Afya, Zahanati na shule za msingi na sekondari ambapo Matanki hayo yatasaidia kwa ajili ya utunzaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa