Changamoto ya Miundombinu ya Barabara pamoja na Mifereji ya maji taka katika Halmashauri ya Manispaa Kigamboni Jijini Dar es salaam imepata mwarobaini baada ya Mradi wa uendelezaji wa miundombinu ya Dar es salaam (DMDP) kutenga fungu maalumu kwaajili ya utatuzi wa Kero hizo
Mkuu wa wilaya hiyo Mh Halima Bulembo ameyasema hayo akiwa kata ya Tungi wakati wa ziara yake maalum ya mtaa kwa Mtaa yenye lengo la kusikiliza na Kutatua kero za wakazi wa Kigamboni ambapo amesema Rais Dkt Samia suluhu Hassan ameidhinisha Mradi huo wa DMDP awamu ya pili na unatarajia kuanza mwezi Octoba hadi Novemba Mwaka huu.
Mhe Bulembo amesema Mradi huo ukitekelezwa utapunguza kwa kiasi kikubwa kutuama kwa maji machafu katika maeneo ya Mitaa mbalimbali ambayo imekuwa kero ya wanakigamboni kwa muda mrefu sambamba na kurahisisha shughuli za kiuchumi kutokana na Barabara Kupitika kwa urahisi
Amesema tayari utaratibu wa awali wa kuanzia mradi huo umefanyika na kilichobaki ni wakandarasi kuanza utekelezaji ambao wataanza na Kilomita 21 za awali.
Pamoja na mambo mengine Bulembo aliwataka wanakigamboni kujiandaa na kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura, zoezi litakalo anza tarehe 11 hadi 20 mwezi oktoba ili watibu haki yao ya kikatiba ya Kumchagua kiongozi wanae mtaka
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa