Dkt. Ndugulile ameyasema hayo leo tarehe 30 Disemba, 2023 katika shughuli ya kupokea magari hayo iliyofanyika katika Ofisi za huduma ya Chanjo zilizopo Mabibo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mbunge Ndugulile ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa hatua za kuimarisha huduma za Afya pamoja na kujenga majengo na kuvipatia vituo hivyo magari hayo na kuweza kutoa huduma bora.
*"Upatikanaji wa magari haya utasaidia sana kuboresha huduma za dharura kwa wagonjwa wa Kigamboni na kuimarisha usimamizi wa huduma za Afya katika Wilaya ya Kigamboni"* Alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa halmashauri ya manispaa ya kigamboni kuyatunza magari haya na kuhakikisha kwamba magari haya yanatumika kwa matumizi yaliyolengwa.
Katika Makabidhiano hayo Mbunge Dkt. Ndugulile amembatana na Dkt. Lucas Ngamtwa - Mganga Mkuu (W) Kigamboni, Dkt. Mohammed Mnyau - Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa