Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri leo ameishukuru kampuni ya KC LAND DEVELOPMENT PLAN CONSULATANT COMPANY LTD kwa msaada wa mifuko ya simenti 100 yenye thamani ya shilingi 1,500,000/= kwa lengo la kuunga mkono jitihada za kuboresha miundombinu ya elimu kwa wananchi wa Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa anawashukuru wadau wa maenedeleo kwa kuweza kuja kuungana na wananchi na viongozi wa kigamboni kwa kuhakikisha guruduma la kutoa elimu bora linafanikiwa na kuongeza kuwa Mpaka sasa changamoto ya vyumba vya madarasa limekwisha changamoto iliyopo ni madawati ambayo nayo hivi karibuni yanatarajiwa kukamilishwa.
Mhe. Sara amesema KC wamekuwa wadau wa kwanza kufunguluia ujenzi wa Shule ya kisasa ya Msingi inayolengwa kujengwa kwenye eneo la makao makuu ya Wilaya Gezaulole ambapo Mkurugenzi amekwisha weka kwenye mpango wa bajeti ijayo.
“Mifuko hii itakwenda kufyatuliwa kwenye kiwanda chetu cha matofali ambapo tunatarajia kupata madarasa matatu, Unapomsaidia mtoto elimu unakuwa umemsaidia yeye pamoja na familia yake, sisi tunawashukuru sana”.Alisema Mkuu wa Wilaya
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bw. Msoses Chilla amesema Mradi huo wa ujenzi wa Shule ya kisasa ya Msingi Gezaulole unatarajiwa hadi kufikia mwezi wa 12 uwe umekamilika ili kuruhusu watoto kuweza kusoma.
Ameongeza kuwa Msaada huo wa mifuko ya simenti umeifungulia njia Kigamboni hasa Taasisi kama KC zinaposhirikiana na Serikali inatoa faraja, hivyo anaendelea kuwakaribisha wadau wengine waweze kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya Elimu na sekta nyingine zote.
Msemaji wa Kampuni ya KC Mussa Hussein amesema kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora na wao kama wadau wameguswa kutoa kidogo walinacho kwani wanatambua kuwa Elimu ni msingi na wanaahidi kuendelea kutoa ushirikiano.
Kaimu Mkurugenzi Bw. Mosses Chilla akishukuru Kc kwa msaada wa Matofali kwa msemaji wa kampuni ya KC
Msemaji wa KC Bw. Mussa Hussein akizungumzia lengo la kutoa msaada huo
Mifuko ya simenti ikishushwa na kuingizwa kiwandani.
Mtambo wa kufyatulia matofali.
muonekano wa kiwanda cha kufyatulia matofali.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa