Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri Leo amewataka wananchi wa Vijibweni mtaa wa Mkwajuni waliokataa kulipwa fidia hapo awali na wale waliolipwa kwa mapungufu kufika ofisi ya Mkurugenzi ili kulipwa fedha zao za fidia ikiwa ni msimamo wa Serikali juu ya mgogoro baina ya wakazi wa eneo hilo na muwekezaji mkorea uliodumu tangu 2004.
Mkuu wa wilaya ametoa msimamo huo Leo alipofanya ziara ya kusikiliza wananchi wa eneo la Mkorea na kuona maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kwenye Daraja la Mwalimu Nyerere na barabara inayounganisha vijibweni na Kibada.
"Naomba mgogoro huu uishe kwa amani na tumruhusu muwekezaji kuendelea na uwekezaji, wale ambao hamridhiki na msimamo huu uliotolewa na Serikali mnaruhusiwa kwenda Mahakamani" alisema Mkuu wa Wilaya.
Wakati huohuo Mhe. Sara amepongeza na kufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara eneo la daraja la Mwalimu Nyerere na ile inayounganisha Kibada na kusema kuwa miundombinu hiyo imezingatia hali ya Kigamboni kwa kuweka mifereji itakayoruhusu maji kupita kuelekea baharini na kuzuia maji kutuama.
Aidha Mkuu wa Wilaya amemtaka afisa ardhi wa Wilaya kufatilia uhalali wa umilikia wa Kiwanja kilichozungukwa na miundom ya makaravati ili kuacha miundombinu hiyo iwe huru na kutumika wakati wowote inapohitajika.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo
mmoja wa mwnanchi akiwasilisha hoja zake kwa Mkuu wa Wilaya alipotoa fursa ya kuwasikiliza wananchi wa Vijibweni juu ya fidia zao.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa