Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri amefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya mifereji ya maji Kata ya Kigamboni kwa lengo la kupata ufumbuzi wa muda mfupi ili kuondoa tatizo la mafuriko pindi mvua zitakapoanza.
Akizungumza kwenye ziara hiyo Mhe. Sara amesema kuwa ametembelea baadhi ya maeneo ameona changamoto ila amebaini kuwa ndani ya wilaya ya kigamboni kuna miundombinu ya maji ya kihistoria ambapo miundombinu hiyo imekufa kwa kutokukarabatiwa, kutofanyiwa usafi na muingiliano wa shughuli za kibinadamu zinazokwamisha maji kupita kuelekea baharini.
Ameongeza kuwa ili kujiepusha na athari za mvua ni lazima kufufua mifereji na kutengeza miundombinu ambayo imakwisha haribiwa ambapo ameagiza wataalamu kutoka manispaa kushiriikiana na uongozi wa Serikali za Mitaa kwa kupita na kubaini maeneo yote ambayo mifereji inapita na kuona namna itakayowezesha kutengeneza mifereji ya muda mfupi ili mvua inapokuja maji yasiweze kutuama.
"Maji yanaingia kwenye hospitali, mahakamani, kituo cha polisi, shuleni na maeneo mbalimbali ya kibishara , mimi kama mkuu wa Wilaya siwezi kusubiri mpate athari ndiyo nije kutoa pole, tuchukue tahadhari mapema, hatuwezi kusubiri mpango wa mda mrefu kutoka Serikali kuu"Alisema Mhe.Sara
Aidha Mhe.Sara aliwahakikishia wananchi wa Kigamboni kwamba yupo tayari kushirikiana nao kwa kutumia wadau mbalimbali kuhakikisha mbadala wa mifereji unapatikana lakini kwakuwataka wananchi nao kujitolea nguvu kazi na kushiriki kwa namna nyingine yoyote pindi watakapohitajika.
"Nipo tayari kusaidia kokoto, mawe, magari ya vijiko na vitu vingine mtakavyohitaji , wananchi watakaokuwa tayari mimi nipo tayari, Kigamboni ndiyo sehemu pekee inayotoa malighafi za ujenzi kwa kiwango kikubwa hivyo siwezi shindwa kuwasaidia"Alisema Mhe. Sara
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya amewataka waendesha bodaboda wa kituo cha machava kufanya usafi kwenye karavati lililopo kwenye eneo hilo ambalo wameligeuza choo na kusema kuwa ikifika jumatatu ijayo hapajasafishwa kituo hicho kitafungwa kwa shughuli za bodaboda.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewakabidhi Tarura karavati lililopo eneo la midizini lililotelekezwa na TANROADS kwa kipindi cha zaidi ya Miaka miwili ili liweze kusaidia kwenye utengenezaji wa mifereji ya kupitishia maji inayotarajiwa kukarabatiwa hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ametembelea maeneo ya Kichanga chui,kituo cha afya Kigamboni, kituo cha polisi na eneo la feri ambapo ziara hii ni endelevu.
Mkuu wa Wilaya akuisaini kitabu cha wageni kata ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akizungumza na baadhi ya wananchi kwenye ofisiza Kata ya Kigamboni.
Mkuiu wa Wilaya na viongozi wengine wakitoka kwenye kituo cha Afya Kigamboni.
Karavati walilopewa TARURA likipimwa na mtaalamu kutoka TARURA huku mkuu wa Wilaya akishuhudia.
Mwananchi wa Kichanga chui akielezea changamoto ya mafuriko wanayokumbana nayo pindi mvua zikianza kunyesha.
Ziara ikiendelea
Katibu Tawala Wilaya Bi. Rahel Mhando akizungumza na wananchi Kata ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa