Mkuu Wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri ametoa rai ya kuhakikisha miradi ya kihistoria inatunzwa na kuenziwa ikiwa ni pamoja na kudumisha mahusiano hususani miradi inayohusisha nchi mbili kama TAZAMA.
Akizungumza kwenye ziara ya kutembelea makampuni ya mafuta na gesi yaliyopo Kigamboni ikiwa ni siku ya pili, Mkuu wa Wilaya alisema anafuraha kufika TAZAMA na amefurahishwa kuona baadhi ya mitambo inafanyiwa ukarabati na kujengwa kwa kuzingatia mradi huo ni wa miaka mingi.
Mkuu wa Wilaya amesema kwakua miradi yoyote lazima ihusishe wadau ambao ni wananchi ni vyema Elimu ikatolewa juu ya Usalama na tahadhari wanayopaswa kuchukua pindi majanga yatakapotokea hususani kwenye miradi ya mafuta na gesi na miradi mingine mikubwa badala ya kusubiri hadi majanga yatokee.
Ameongeza kuwa ziara inayofanyika itakua ni ufunguo kwa wakazi wa Kigamboni kwanza Kwa kuweka mahusiano mazuri na wamiliki Wa kampuni, kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji wa makampuni kwa kupata ajira rasmi na zisizo rasmi ili kufanya mzunguko wa Fedha kuwa mkubwa hatimae kuongeza kipato.
Ziara imelenga kusikiliza changamoto za makampuni na kuzipatia ufumbuzi ngazi ya Wilaya na kuzipeleka ngazi za juu pale itapobidi, kuhamasisha utoaji Wa Elimu wwa wananchi namna ya kuchukua tahadhari na Usalama na kuhakikisha wananchi wananufaika na uwekezaji wa makampuni haya kijamii.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye ofisi za TAZAMA
Mhandisi Patric Mzava wa TAZAMA akionesha namana matanki ya mafuta yanavyoundwa walipoingia kwenye tanki moja wapo kutembelea
ukaguzi wa moja ya mitambo ya TAZAMA
Baadhi ya Mitambo ya mafuta.
Kamati ya ulinzi na usalama walioketi wakisikiliza historia ya TAZAMA na waliosimama ni wafanyakazi wa TAZAMA.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa