Mkuu wa wilaya ya kigamboni amepongeza ujenzi wa kituo cha afya kimbiji na kutesema kuwa muundo wa majengo kwa kuongeza vyumba sita haufanani na kituo chochote nchi nzima hivyo kitakuwa ni kituo cha mfano huku akipongeza pia hatua za ujenzi wa hospitali ya Wilaya iliyoanza kujengwa.
Akizungumza leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa kituo cha afya kimbiji na hospitali ya wilaya inayojengwa somangila, Mhe.Sara amesema anaishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwaboreshea wananchi huduma za Afya hususani kwa Wilaya hii mpya ya Kigamboni ambayo bado ndio inakua.
" Nawapongeza kamati na uongozi mzima kwa kufanikisha ujenzi wa kituo hiki ambacho hapo awali kilitaka kuonesha kwamba kigamboni hakuna usimamizi mzuri, majengo yanapendeza huduma zinaboreshwa, tuwahamasishe wananchi kuja kutibiwa hapa lakini pia watumishi wawajibike katika kutunza mazingira haya kwa kupanda miti ambayo mimi nitashiriki kuileta" alisema Mhe.Sara
Aidha akizungumzia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Mhe.Sara amesema kuwa Kigamboni ni miongoni mwa Halmashauri ambayo imepewa fedha kiasi cha bilioni 1.5 na kwamba ipo kwenye orodha ya Halmashauri 15 ambazo zimethubutu kuanza ujenzi kwa haraka na zinafanya kazi vizuri, tofauti na Halmashauri nyingine ambazo bado wanasafisha maeneo na wengine wakihangaika kutafuta maeneo.
Hadi kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya kimbiji kiasi cha milioni 455 zimetumika ambapo milioni 400 kutoka Serikali kuu na Milioni 55 kutoka Manispaa kwasasa huduma za uzazi na maabara tayari zimeanza kutolewa.
Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unatarajiwa kukamilika june 2019 na majengo yaliyopangwa kujengwa ni utawala, wazazi, OPD,mionzi,maabara, stoo ya dawa na chumba cha kufulia nguo.
Msafara wa Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri kushoto ukiongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dk.Charles Mkombachepa wakitoka kuangalia jengo la m,ama na mtoto kituo cha afya Kimbiji.
Mkuu wa Wilaya kushoto kiongozwa na Mganga Mkuu wakifurahia huduma ya vitanda kwenye jengo la mama na mtoto.
muonekano wa ndani jengo la mama na mtoto
Mganga Mkuu Dk. Charles Mkombachepa kulia akitoa maelezo ya baadhi ya vifaa ambavyo tayari vimeletwa na MSD kwaajili ya kutolea huduma.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri (katikati) akitoa maelekezo ya uboreshwaji wa mazingira ya kituo cha afya kwa kupanda miti na maua.
wataalamu mbalimbali wakiwa wameambatna na Mkuu wa Wilaya wakikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa Kata ya Somangila
mafundi wakiendelea na ujenzi wa msingi jengo la utawala la Hospitali ya Wilaya.
Mkuu wa Wilaya akisoma ramani ya Majengo ya Hospitali ya Wilaya inayojengwa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa