DC FATMA A .NYANGASA AWATAKA WALEZI WAKAWE MABALOZI KWENYE JAMII CHANJO YA POLIO
Hayo yamejiri Leo katika Hospitali ya Vijibweni ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Fatma Almas Nyangasa amewataka walezi na wazazi walioshiriki katika Uzinduzi huo kwenda kuwa mabalozi katika jamii na kuwaelimisha wengine juu ya umuhimu wa chanjo ya Polio kwa ajili ya afya ya watoto.
DC Nyangasa amesema serikali imewekeza katika afya na imeendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuweka nguvu katika kuwezesha chanjo hii hivyo wanakigamboni tunaendelea kumshukuru Mh.Rais Samia Suluhu Hassan katika hili.
Aidha amewataka walezi na wazazi kudumisha usafi katika majumba yao kwani uchafu ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu wa polio ambao huambukiza na kupelekea mtoto kupooza.
Kuhusu utekelezaji wa zoezi hili la chanjo DC Nyangasa amesema tayari kuna timu ya watu 59 ambao wapo katika makundi ya watu watatu watatu watapita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo hivyo wawatoe watoto wao waweze kupata chanjo,sambamba na hili amewataka wasisite kuuliza maswali pale wanapotaka kufafanuliwa jambo lolote na kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake katika Jambo hili hivyo tusaidie katika kuona jambo hili linafanikiwa.
"Hili ni Jambo letu wote tuhakikishe watoto wamepata chanjo na kufanya taifa kuwa na kizazi salama."alisema Mh.Nyangasa.
Katika zoezi lililopita Wilaya ya kigamboni ilifanikiwa kuvuka lengo Kwa kuchanja watoto 37000 tofauti na lengo walilojiwekea la watoto 30000.Shime wazazi tuwatoe watoto wapate chanjo kuepuka madhara ya polio.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini KMGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa