Mkuu wa wilaya ya Kigamboni mh. HALIMA Bulembo amekutana na baraza la ushauri la wazee kwa lengo la kupata ushauri, kusikiliza changamoto pamoja na kujua mambo kadha wa kadha yahusuyo wazee.
Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kepteni mstaafu Samweli Ngasa amewasilisha changamoto ya miundo mbinu ya bara bara ikiwemo ukosefu wa mitaro ya kupitisha maji machafu
Aidha Brigedia mstaafu Haroon Othumani Mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya amemuomba Mkuu wa Wilaya kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa kuwepo na ushiriki rasmi wa wazee katika vikao vya Baraza la Madiwani ili waweze kupata wasaa wa kutoa mawazo yao.
Akijibu hoja ya kutoshirikishwa kwenye vikao vya baraza Mh. Bulembo alisema "Nitamuelekeza
Mkurugenzi kusimamia swala la wazee kushiriki vikao vya mabaraza ya Madiwani, kwa kuwa si jambo kubwa sana na wala halitagharimu chochote zaidi uwepo wenu utatuongezea maarifa ndani ya mabaraza hayo"
Akimalizia Mh Mkuu wa Wilaya aliwataka wazee kuwa na subra wakati akiendelea kufanyia kazi changamoto zote walizowasilisha ikiwemo kuongezewa idadi ya wazee wanaotakiwa kupatiwa kadi za matibabu.
Mkuu wa wilaya ameendelea kufanya vikao na viongozi wa makundi mbali mbali ambapo anatarajia kukamilisha ratiba hiyo ifikapo Februari 24, 2023.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa