Hayo yamejiri leo 19/7/2023 katika ziara yake ya utatuzi wa Kero katika Kata ya Tungi ambapo ameweka wazi kuwa serikali ya awamu ya sita inajikita katika kutatua kero mbalimbali zikiwepo za sekta ya Elimu ambapo katika mwezibwa sita tayari wilaya ya Kigamboni imepokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu ili kuondoa kero ya wanafunzi kujaa kupitiliza katika madarasa.
Amesema Kigamboni imepokea kiasi cha shilingi milioni 528 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Lingato katika Kata ya Kisarawe II ,utekelezaji wa mradi huu ni kupitia uboreshaji wa elimu ya sekondari (SEQUIP).
Aidha bilioni 1.5 ambazo zitajenga shule ya Mkoa wa Dar es salaam katika wilaya ya Kigamboni kwenye eneo la Halmashauri Kata ya Somangila nazo zimepokelewa, mradi huu pia ni kupitia uboreshaji wa elimu ya sekondari ( SEQUIP )
Sambamba na hilo zimetolewa shilingi mil.470 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Tundwi Songani katika Kata ya Pembamnazi ikiwa ni kupitia mradi huo wa SEQUIP.
Vilevile pesa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu milioni 95 zimeshapokelewa ambapo zitajenga nyumba mbili za walimu katika Kata ya Pembamnazi zitakazokuwa katika mtindo wa nyumba mbili kwa moja . .
Mh.Bulembo amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiletea fedha za miradi Kigamboni kwa ajili ya kuboresha elimu na sekta ya Afya,barabara ,maji n.k. .
Mhe.Halima Bulembo ameendelea na ziara yake ya kutatua kero mtaa kwa mtaa ambapo kesho 20/7/2023 atakuwa katika Kata ya Kigamboni kusikiliza na kutatua kero za wananchi ,wote mnakaribishwa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa