Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo ameendelea na ziara yake ya kutambua kero za mtaa kwa mtaa ambapo leo tarehe 14 Juni, 2023 amefika katika mitaa ya Mikenge,Kizito huonjwa na Ngobanya ndani ya Kata ya Kimbiji.
Katika kutatua changamoto za Wananchi, DC Bulembo ameweka wazi hatua zilizofikiwa ili kumaliza mgogoro wa barabara ya Kidagaa ulikuwa kati ya Wananchi na Mwekezaji Kampuni ya (ASM Limited) mgogoro ambao umedumu kwa muda mrefu.
" *Tumefikia jitijhada kubwa sana haikuwa rahisi, niwaombe wana Mikenge mridhie tumepata barabara tatu tofauti zitakazokuwa zinaenda mpaka ufukweni na kwenye makazi ambapo mwanzo barabara ilikuwa moja, niwasihi tusiwe na migogoro baina yetu kama Serikali, Wananchi na Wawekezaji, tuliongea na Mwekezaji (ASM) na yeye amekubali kuwajibika katika kutengeneza barabara itakayopita hadi baharini na tulimpa muda wa siku 90 atakamilisha* " Alisema DC Bulembo
Aidha DC Bulembo amemtaka Afisa Ardhi Manispaa ya Kigamboni kuwaandikia barua wawekezaji wote za kuwataka kuzingatia sheria na taratibu kwa kushirikisha serikali kupitia idara ya ardhi kwenye masuala ya tathmini kwa maeneo wanayonunua kwa wananchi ili kuepukana na migogoro mbalimbali kama dhulma.
Akijibu kero ya vyoo shule ya Msingi Mikenge DC Bulembo ameahiza Manispaa kumleta Mhandisi wao kufika katika shule ya Mikenge kuona adha inayolalamikiwa ya ubovu wa vyoo ilikusudi kujua namna gani ya kuweza kurekebisha vyoo hivyo.
Nae Afisa elimu Msingi ndg.Hasaan Mianza ameweka wazi kwa wananchi( walipotaka kujua kuhusu kuongezwa kwa madarasa na uhaba wa walimu) kuwa zipo fedha kutoka kwenye Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 zimetengwa kiasi cha Tsh Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa mawili katika shule ya msingi Mikenge, Aidha katika ajira mpya zilizotangazwa, Manispaa imeweka kipaumbele cha kuongezwa kwa walimu wawili katika shule hiyo.
Akijibu maswali ya Wananchi, Meneja DAWASA amesema katika bajeti ya 2023/24 zimetengwa fedha na kuanzia mwezi wa 9 ujenzi wa kupitisha mabomba ya maji safi kwa kilomita 5 utaanza n
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa