Mkuu wa Wilaya kigamboni Mh. Halima Bulembo amemtaka Mkurugenzi Mtendaji kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa Dampo la kisasa kuanza mara moja kama ilivyopangwa.
Hayo ameyasema leo Juni 21,2023 wakati akifunga ziara yake ya mtaa kwa mtaa katika mtaa wa Kigogo uliopo kata ya Kisarawe 2
DC Bulembo amesema Mkurugenzi Mtendaji kwa kushirikiana na Idara ya Mazingira hawana budi kuweka mpango mkakati wa kuwezesha ujenzi wa Dampo la kisasa ili kupunguza adha ya uchafu kwa wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo.
"Maelekezo yangu kwa Mkurugenzi utekelezaji wa ujenzi wa Dampo la kisasa uanze haraka ili kupunguza Adha kwa wakazi wa eneo hili" Alisema.
Sambamba na hilo Mh Bulembo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kutupa taka hovyo huku akiwasihi wataalam kutoka Idara ya mazingira kutembelea maeneo ya Dampo mara kwa mara kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna bora ya utunzaji wa mazingira.
Sambamba na hilo DC Bulembo amepiga marufuku uchimbaji wa madini ya mchanga usiofuata taratibu kwani ni kosa kisheria na yeyote atakaye bainika kukiuka katazo hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa