Mkuu wa Wilaya ya kigamboni Mh. Halima Bulembo amewataka wananchi kushiriki katika ujenzi wa miundo mbinu hususani vyumba vya madarasa.
Hayo ameyasema leo Juni 19, alipowasili katika mtaa wa Ngoma Mapinduzi uliopo kata ya Kisarawe 2 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Mtaa kwa Mtaa.
Mh Bulembo amesema Serikali inaendelea kutekeleza ujenzi wa miundo Mbinu ndani ya Wilaya ya Kigamboni na mpaka kufikia june 2023 tayari imepokelewa zaidi ya shilingi bilioni 1.9 kupitia mradi wa BOOST.
"Niwaombe tutoe maeneo na tushiriki kwenye ujenzi wa madarasa ili inapotokea serikali inatuletea fedha wataalam wazielekeze maeneo ambayo tayari wananchi wamewekeza nguvu zao"
Aidha Diwani wa kata ya Kisarawe 2 Mhe. Issa zahoro amewasitiza wazazi kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu kwa kuwa tayari Serikali inaendelea kujenga miundo mbinu ambayo ni rafiki kwa watu wenye mahitaji maalum.
"Tusiwafungie watoto wenye mahitaji tukidhani kuwa tayari wameshapoteza kwenye maisha, tuwapeleke shule
kwa sababu kuna bweni linalohudumia watoto wenye mahitaji lipo shule ya msingi Chekeni mwasonga iliyopo hapa Kisarawe 2" alisema Mhe. Zahoro.
Kiasi cha takribani milioni 120 zimetolewa kujenga bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa TEHA mil 70 na mapato ya ndani Mil. 50.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa