Mkuu wa wilaya Kigamboni Mh. Halima Bulembo leo Februari 23,2023 amekutana na Watendaji wa Kata zilizopo Manispaa ya kigamboni kwa lengo la kufahamiana sambamba na kupeana uzoefu kulingana na majukumu wanayoyatekeleza kwenye kata zao
Akizungumza wakati wa kikao Mh. Bulembo aliwataka Watendaji wa kata kushirikiana na watendaji wa mitaa ili kupunguza na kumaliza kabisa migogoro ya Ardhi ambayo imekua changamoto kubwa ndani ya Wilaya hiyo.
Sambamba na hilo Mh. Mkuu wa Wilaya aliwaonya watendaji kutojihusisha katika kuitengeneza migogoro ya ardhi ikiwemo kushiriki katika uaandaaji wa taarifa zinazopelekea mtu kupata hati ya umiliki wa eneo ili hali wanafahamu ubatili wa mauziano hayo.
Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya aliwataka watumishi hao kuwa daraja kati yao na wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayoletewa fedha kutoka Serikali kuu pamoja na miradi yote ambayo inatekelezwa kutokana na fedha za mapato ya ndani.
Akijibu hoja iliyotolewa na Mtendaji Kata ya Pemba Mnazi David Basil ya kutaka kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara juu ya usimamizi wa miradi na utawala bora. Mh. Bulembo ameahidi kulisimamia na kuwapatia fursa za kushiriki mafunzo hayo kadri ya upatakanaji wa fedha.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa