Na. Minde Honorata
Mkuu waWilaya ya Kigamboni Mh. Halima Bulembo amewataka wanawake wa wilaya hiyo kuachana na mikopo inayojulikana kama "kausha damu".
Hayo ameyasema leo wakati akijibu moja ya kero iliyowasilishwa na mwananchi wa kata ya vijibweni Bi. Hidaya Kundi aliyezilalamikia taasisi za mikopo ambazo zina riba kubwa na zisizo rafiki.
Mh. Bulembo amewataka wananchi kujenga tabia ya kufuatilia taarifa za mikopo nafuu na isiyo na riba inayotolewa na Serikali kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri.
" Niwaombe mfike ofisi ya kata muonane na afisa maendeleo awape utaratibu mzuri utakaowawezesha kupata mikopo inayotolewa na Serikali isiyo na riba.
Sambamba na hilo Bulembo amewataka wananchi waliokopa kwenye hizo taasisi kulipa madeni yao yote kabla ya kuachana nayo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa