Dc Bulembo ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo tarehe 25/02/2023 katika zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi lililofanyika katika Mtaa wa Mjimwema kata ya Mjimwema. Ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Amos Makala la kuhakikisha kila wilaya ya mkoa wa Dar es Salaam inashiriki usafi wa mwisho wa mwezi kwa lengo la kuhakikisha mkoa unakuwa msafi.
Aidha Dc ametoa rai kwa wananchi ambapo ameeleza kuwa zoezi la usafi ni la lazima na sio la hiari hivyo amewataka kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi muda wote.
Kwa upande mwingine Mstahiki Meya Manispaa ya Kigamboni Mheshimiwa Ernest Ndamo Mafimbo amewataka viongozi wa Mitaa yote ya Manispaa ya Kigamboni kuhamasisha Wananchi katika maeneo yao ya kazi kwa lengo la kuhakikisha wanachi wanapata mwamko wa kufanya usafi.
Aidha aliwashukuru wakazi wa Mjimwema kwa ushiriki wao katika usafi na kuwataka kuendelea na moyo wa kujitokeza pale mazezi na shughuli mbalimbali zinapojitokeza.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa