Mhe. Halima Bulembo ametoa wito huo leo Machi 12. 2025 katika hafla fupi ya kupokea vifaa tiba vya kutolea huduma ya Afya ya uzazi vyenye thamani ya Tsh Mil 23 vilivyotolewa na wanawake wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) ikiwa ni mchango wao katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
"Natoa pongezi kwa wanawake wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia wananchi wa Kigamboni vifaa hivi vitaenda kusaidia utoaji wa huduma ya Afya pale penye upungufu." Amesema Mhe Halima Bulembo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja Rasilimali watu wa Mamlaka ya bandari Bi. Mwajuma Mkonga amesema wametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia wanawake wanaokuja kupata huduma ya uzazi katika Hospitali ya Wilaya.
Aidha Amesema Mamlaka imetoa vifaa hivyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya Sekta ya Afya.
Baadhi ya aina 15 ya vifaa tiba vilivyotolewa na wanawake wa Mamlaka ya usimamizi wa bandari ni pamoja na taa za uchunguzi, kitanda cha kubebea wagonjwa, mzani wa mtoto, kipimo cha oksijeni, mashine ya kupima sukari kwenye damu, kipimo cha oksijeni, skrini ya wagonjwa sabuni, mashine ya kutengeneza oksijeni, stendi ya chupa ya drip pamoja na nepi za watoto.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa