Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo ameongoza kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika leo Februari 18 2025 katika ukumbi wa Ofisi yake kwa lengo la kujadili shughuli mbalimbali za lishe za robo hiyo.
Akiwasilisha taarifa utekelezaji wa shughuli hizo Afisa lishe wa Manispaa ya Kigamboni Bi. Anna Byashara amesema kamati imefanikiwa kutoa elimu ya lishe kwa wapishi wa shule 8 za Sekondari za Manispaa ya Kigamboni huku wakihimizwa kuweka virutubishi kwenye vyakula wanavyoviandaa.
Aidha kamati imetoa wito kwa shule za Sekondari za binafsi na Serikali kuanzisha bustani za mbogamboga ili kutoa elimu ya lishe kwa wanafunzi huku wakiwafundisha stadi za maisha.
Sambamba na hilo imetoa elimu kwa wafugaji wa kuku kuacha tabia ya kutumia madawa ya antibayotiki ili kupunguza usugu wa vimelea dhidi ya dawa kwa binadamu na wanyama hasa ukizingatia kuwa nyama ya kuku wa kisasa inaliwa kwa kiwango kikubwa katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha imefanikiwa kuanzisha kamati za makao katika vituo vya kulelea watoto yatima ili kuboresha utoaji wa huduma katika vituo hivyo
Kamati ya lishe huketi mara 4 kila mwaka ili kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa hali ya lishe kwa Wananchi wa Manispaa ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa