Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Kigamboni (DCC), ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mheshimiwa Halima A. Bulembo, ameongoza kikao maalum cha kujadili na kupitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe kutoka makundi mbalimbali, wakiwemo wakuu wa idara wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, wakuu wa taasisi za serikali wilayani humo, wawakilishi wa vyama vya siasa, watendaji wa kata, madiwani, pamoja na viongozi wa asasi za kiraia.
Katika mjadala huo, wajumbe wamejadili kwa kina mpango huo wa bajeti, wakizingatia vipaumbele vya maendeleo ya Kigamboni, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu, elimu, afya, na huduma za kijamii. Hatimaye, kikao kimepitisha na kukubaliana na Rasimu ya Mpango wa Bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, hatua inayotarajiwa kuleta maendeleo chanya kwa wakazi wa Kigamboni.
Mheshimiwa Bulembo amepongeza ushirikiano wa wadau wote waliohudhuria kikao hicho na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa bajeti hiyo kwa ufanisi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na maendeleo endelevu
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa