*DC BULEMBO AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KUNDI LA WAENDESHA BODABODA NA BAJAJI, ATOA SALAMU ZA RAIS SAMIA KATIKA KUWATHAMINI - KIGAMBONI*
> _Waweka mikakati ya kuhakikisha wanafanya biashara zao kwenye mazingira mazuri na usalama_ .
" *Nimeona ni vema nikutane na kundi hili nijitanbulishe kwenu kwa lengo la kufahamiana, tunapoletwa viongozi katika Wilaya zetu tunaletwa mahususi kuwasaidia nyie Wananchi kwa makundi mbalimbali, mfano leo una bodaboda moja tukurahishie mazingira yako na usalama wako ilikusudi kesho na keshokutwa uwe na mafanikio upate na ya pili* "
" *Katika vikao vyetu tunavyokuwa tunafanya, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatusisitiza na kuweka kipaumbele kwenu kwamba anatambua umuhimu wa jamii yetu ya waendesha pikipiki (bodaboda) na bajaji na anawathamini sana na kwa nafasi kubwa sana changamoto ambazo mnazipitia zinafanyiwa kazi kwasababu ni kundi ambalo linainua uchumi wa Nchi kupitia mtu mmoja mmoja* "
" *Niendelee kuwasisitizia kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia anawathamini, anawajali, anawapenda na mimi kama msaidizi wake katika Wilaya hii nipo kutekeleza hilo, naombeni ushirikiano wenu wa kuhakikisha mnaendelea kuzingatia na kufuata sheria za usalama wa barabarani* "
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo, alipokaa kikao na kundi la waendesha Bodaboda na Bajaji wa Wilaya ya Kigamboni katika ukumbi wa CCM Kigamboni tarehe 21 februari, 2023.
#KigamboniMpya
#KaziIendelee
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa