Mkuu wa wilaya kigamboni Halima Bulembo amewataka wananchi kushiriki shughuli za ulinzi shirikishi ili kutokomeza tatizo la wizi kwa wakazi wa Kigamboni.
Hayo ameyasema leo Juni 20, 2023 alipokua akihutubia katika kikao cha Wananchi cha utatuzi wa kero katika mtaa wa Sharifu, Mwaninga, Mwasonga iliyopo kata Kisarawe 2.
Mh. Bulembo amesema kuwa kila Mwananchi ana wajibu wa kuwa mlinzi wa mali za mwingine na hiyo itatekelezwa endapo tu wananchi watashiriki katika ulinzi shirikishi unaojulikana kama Sungu Sungu.
"Niwaombe vijana, nyinyi ndo walinzi wa amani katika maeneo yetu tunayoishi tuweke utaratibu mzuri kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya kata na vile vilivyopo ndani ya mitaa yetu," alisema Bulembo.
Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo kulielekeza Jeshi la polisi kuruhusu vituo vyao kufanya kazi masaa 24 ili kuwezesha shughuli za ulinzi na usalama kufanyika kwa weledi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa