Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri amemuweka ndani (masaa 24) msimamizi wa ujezi wa ukuta wa kampuni ya Afroil ,Mhandisi Vilelian Magembe mwenyewe kampuni ya ujenzi ya NECO CONTRACTORS kwa kukaidi kusitisha ujenzi wa ukuta unaojengwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara baada ya Mkuu wa Wilaya kusitisha ujenzi huo jana alipotembelea kwenye kampuni hiyo.
Akizungumza leo kwenye kampuni ya Afroil Vijibweni, Mkuu wa Wilaya amesema kuwa eneo linalojengwa halina kibali pia linaonekana kuwa ni hifadhi ya barabara na hivyo kuwataka kupeleka nyaraka zinazowaruhusu kufanya ujenzi kwenye eneo hilo na kibali walichopewa lakini pia kusitisha ujenzi huo mpaka pale agizo litakapotolewa.
“wamekaidi kuacha ujenzi, mafundi wanaendelea na ujenzi, nyaraka mmezileta leo ofisini lakini tamko lakuendelea na ujenzi sijalitoa, nakuweka ndani masaa 24, lazima utaratibu ufuatwe kama wawekezaji ili kuepuka malalamishi na migogoro inayoweza kuzuilika kwa kutii sheria” alisema Mkuu wa Wilaya.
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema wataalamu wanaohusika na kutoa vibali wanatakiwa kuangalia na maeneo ya uwekezaji kabla ya kuvitoa ili kujua shughuli zitakazofanywa , kubaini kama hazina uharibifu wa miundombinu kwa kufuata sheria badala ya kuvitolea wakiwa ofisini hususani kwenye miradi mikubwa kama ya mafuta .
“Nimebaini mapungufu kwenye utoaji wa vibali, mimi kama Mkuu wa Wilaya nitandaa kikao cha dharula kwasababu hii ni hasara kwanza kwa wawekezaji, unaharibu wa ramani za mipangomiji na mazingira ya rushwa, haiwezekani mtu anajenga vibali afate baadae” aliongeza Mkuu wa Wilaya.
Ziara hii ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea wawekezaji wa mafuta na gesi waliowekeza Wilayani Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Sara Msafiri akizungumza na waandishi kuhusu ufuataji wa sheria za kufuatwa na wawekezaji.
mafundi wakiondoka eneo la ujenzi mara baada ya kusitishwa kuendelea na ujenzi.
baadhi ya Kuta zinazojengwa
Baadhi ya Kuta
Baadhi ya Kuta
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa