Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri ametaka walengwa wa chanjo ya Surua-Rubella na Polio kufikiwa kwa kupatiwa elimu ya umuhimu wa kupata chanjo hizo ili kuhakikisha lengo lililokusudiwa na Serikali linafikiwa .
Akizungumza wakati wa utolewaji wa mafunzo shirikishi kuhusu kampeni ya SURUA-RUBELLA yaliyotolewa leo kwa kamati ya Afya ya msingi ya Wilaya kwenye ukumbi wa mikutano ofisini kwake Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Serikali inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha inadhibiti magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ili kuokoa maisha ya watoto na kuboresha Afya kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa chanjo hizo zinafaida yake na ndiomaana Serikali inapambana kuhakikisha wananchi wanapatiwa hivyo ni jukumu la wanakamati wa Afya kuhakikisha elimu hiyo inatolewa ipasavyo na kuwafikia wote waliokusudiwa ikiwa ni pamoja na kushirikisha makundi mbalimbali.
Akizungumza wakati wa mafunzo Afisa Afya wa Wilaya Bi.Maua Hageshi amesema kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau imeandaa kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo za Surua,Rubella na PolioAmbapo Kampeni hii inalenga watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano kupewa chanjo hizo.
Lengo mahususi la kampeni hii ya kitaifa ni kuzuia na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambayo ni ugonjwa wa Surua, Rubela na Polio kwa kutoa chanjo kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 na kuongeza kinga kwa watoto wote kwa kuwapatia chanjo hata kama wameshapata chanjo hizo katika utaratibu wa kawaida wa kutoa huduma za chanjo
Halmashuri ya manispaa ya kigamboni inatarajia kuchanja watoto wapatao 26711 kwa chanjo ya surua rubella na watoto 15281 kwa chanjo ya polio ya sindano ambapo Jumla ya vituo vitakavyotoa huduma hii ya chanjo ni 25 na zoezi hili linatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe 17-21/10/2019.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa