Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla ameuagiza uongozi wa DAWASA kusimamia Mkandarasi anayesimika mabomba ya kusambaza maji kufanya kazi usiku na mchana ili kuendana na matumaini waliyoyatoa kwa wananchi ya kufikishia maji maeneo ya Wilaya ya Kigamboni na Ilala kuanzia Jumatatu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wake.
Mhe Makalla ameyazungumza hayo leo alipokuwa kwenye ziara yake ya kutembelea visima vya maji vya Kigamboni na kuzindua zoezi la kuwasha maji ya kisima kinachoitwa K11 kinachopeleka maji hayo kwenye Tanki Kuu lenye uwezo wa kuchukua lita milioni 15 za maji lililojengwa Kisarawe II Kigamboni. Pia aliwaeleza wananchi kuwa Serikali inachukua hatua zikiwemo za dharula na za muda mrefu kukabiliana na upungufu wa maji.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa Rais alitoa maelekezo wakati anashughulikia changamoto ya maji, kuwa mradi wa Kigamboni ukamilike kwa haraka kwani alishaidhinisha kiasi cha Bilioni 23 ili kukamilisha mradi kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa maji unaojitokeza kwasasa baadhi ya maeneo.
Aidha ameupongeza uongozi wa DAWASA kuanzia Mkurugenzi,Mwenyekiti wa bodi na watendaji kwa kazi nzuri waliyoifanya, amethibitisha kuwa wanaweza kusimamia na matokeo yake yameonekana.
Ameongeza kuwa Rais anaendelea kuchukua hatua,mchakato wa kupata mkandarasi wa kujenga bwawa la kidunda ambalo kwa kiasi kikubwa litamaliza changamoto ya maji amepatikana na wakati wowote ataanza kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema kuwa anaishukuru sana Serikali kwa kusaidia na kuiwezesha DAWASA kuweza kukabiliana na changamoto hizo ambazo zimekuwepo na wao kama viongozi wanaendelea kuzitatua hatua kwa hatua.
Mkurugenzi wa DAWASA Eng.Cyprian Luhemeja amesema kuwa kuna visima 7 ambavyo vimekamilika vyenye uwezo wa kutoa lita milioni 70, Mahitaji ya Kigamboni na Ilala ni chini ya milioni 70 hivyo wanaamini baada ya mradi kukamilika changaomoto ya maji kwenye maeneo haya ya Ilala, Kigamboni, Temeke na Kurasini itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakifurahi kwa pamoja mara baada ya kuwasha maji kwenye kisisma cha K11
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza baada ya kutembelea mradi wa tanki kuu.
Tanki kubwa la maji linalokusanya maji kutoka kwenye visima 12 vilivyojengwa Kigamboni.
Mkurugenzi wa DAWASA Eng.Cyprian Luhemeja akielezea njia zitakazopita mabomba ya maji yanayojengwa ili kuzifikia Wilaya nyingine za Ilala na Temeke.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla akiwa ameambatana na viongozi wengine wakielekea kutazama namna maji yanavyoingia mara baada ya kuwasha kutoka kwenye kisima cha K11.
.Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Amosi Makalla akiwa ameambatana na viongozi wengine wakishuka kutoka kwenye tanki kuu mara baada ya kutazama namna maji yanavyoingia baada ya kuwasha kutoka kwenye kisima cha K11
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa