TIMU YA MENEJIMENTI YA MANISPAA KIGAMBONI WAKAGUA MIRADI 3 YENYE LENGO LA KUONGEZA MAPATO ILI KUJIONEA HATUA UTEKELEZAJI ZINAZOENDELEA
Hayo yamejiri 6/9/2022 ambapo timu ya Menejimenti ya Manispaa ya Kigamboni wamekagua miradi yenye lengo ya kuiongezea Manispaa hiyo mapato itakapokamilika.
Miradi hiyo ni ujenzi wa Soko la mazao linalojengwa katika kata ya Somangila ambapo mpaka kukamilika kwake jumla ya Tshs.milioni 100 zitatumika mpaka sasa imeshatoa mil.50 za mapato ya Ndani na tayari kiasi kilichobaki kimeingizwa katika bajeti ya 2022/2023.Litakapokamilika soko hili litaiongezea halmashauri mapato kupitia ushuru utakaokuwa unalipwa na wafanyabiashara watakaokuwa wanatunia soko hili, pamoja na kusogeza huduma Kwa wananchi wa eneo hili ambao hawana huduma ya Soko.
Mradi mwingine uliokaguliwa ni mradi wa ujenzi wa Machinjio ambapo mradi huu Hadi Kwisha kwake utagharimu Tshs.mil 180 katika awamu ya Kwanza tayari millions 80 zimeshatolewa .Mradi huu utakuwa na uwezo wa kuchinja ng'ombe 20 mpaka 30 kwa siku.Chanzo cha pesa ni mapato ya ndani ya Manispaa
Pamoja na hiyo mradi mwingine uliyokaguliwa ni mradi wa ujenzi wa sehemu ya abiria kupandia daladala (shade)katika stendi inayotarajiwa kujengwa katika eneo la NAFCO ambapo kutokana na mahusiano mazuri ya Manispaa na wadau wa Kigamboni Kampuni ya Lake Cement wamejitolea kujenga sehemu hiyo kwa nia ya kurudisha huduma kwa jamii na kuonyesha mchango wao kama sehemu ya kuwajibika kwa jamii inayowazunguka.
Akiongea kiongozi wa timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ambaye ni Kaimu Mchumi kwa niaba ya Mkurugenzi bi.Eutropia Mlela amesema wameridhishwa na maendeleo ya miradi waliyokagua kwa kumekuwa imepiga hatua nzuri ya mwendelezo tofauti na walipokagua mara ya mwisho. Wamewashukuru Mkurugenzi na wasimamizi wa Idara husika kwa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi hiyo yenye lengo la kuongeza tija katika kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Manispaa,lakini pia kuongeza huduma bora Kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Tawala CCM.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa