NA: Alda Sadango
Naibu waziri wa Elimu Mhe.Omary Juma Kipaanga leo amefanya ziara ya kutembelea chuo cha Wananchi maarufu kama Anatoglo kinachojengwa katika Wilaya ya Kigamboni na kutarajiwa kumalizika mwezi wa kumi na mbili na kueleza namna Rais alivyojipanga kuimarisha Sekta ya Elimu kwa wananchi.
Waziri kipanga amesema kuwa chuo hicho kilikua kinatoa huduma zake Anatoglo lakini kwa sasa kitahamishiwa Wilaya ya Kigamboni kutokana na ufinyu wa eneo na ameona maendele ya mradi huu yanaonekana kuwa mazuri kwa kiasi hivyo kuonesha matumaini ya kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Aliongeza kwa kusema kuwa katika kuchangia ukuaji wa Sekta ya Elimu Rais Samia Suluhu Hassani alitoa fedha kiasi cha bilioni 6.8 kutoka kwenye fedha ya uviko kwaajili ya ununuzi wa vifaa kwaaajiili ya vyuo vya FDC hivyo chuo hiki kitakapokamilika kitaweza kutumika maramoja sababu vifaa tayari vipo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa ameshukuru Rais Samia kwa kutoa kaisi cha Milioni 690 itakayowezesha kukamilisha ujenzi wa chuo hicho cha Wananchi maarufu Anatoglo na kusema kuwa ni suala la kujivunia sana kwani ,hadi kukamilika kwa awamu hii ya kwanza kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 ambao wataweza kupatiwa mafunzo ya kozi mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa hapo .
Ameongeza kuwa Vijana wengi wameshapitia kwenye chuo hicho nab ado kitaendelea kuwasaidia watu watakaomaliza elimu mbalimbali kuweza kupata mafunzo hivyo anamshukuru Raisi kwa kuelekeza fedha hizo Kigamboni kwani ujenzi wa miradi mbalimbali inayojengwa inaisaidia Kigamboni kukua kulingana na mahitaji halisi ya wananchi.
“Niwaambie wanakigamboni hii ni fursa kwetu na wananchi wengine walio karibu kuja kupata huduma ya mafunzo mbalimbali hivyo tutumie vyema fursa hii ambayo imetufikia” Alisema DC Fatma.
Mkandarasi anayehusika na ujenzi wa chuo hicho amesema uwa kutembelewa na kiongozi kama Naibu waziri kunatia moyo na kuahidi kuhakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa ili kuweza kukamilisha mradi huo kwa umuda uliopangwa.
Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Omary Kipanga akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga chuo hicho , pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa.
Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Omary Kipanga akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa na wataalamu wengine kwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Omary Kipanga akiwa amembatana na wataalamu wengine wakitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.
Hatua ya jenzi iliyofikiwa mpaka sasa kwa moja ya jengo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa