Katika kukamilisha ufungaji wa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioisha june, leo Baraza la Madiwani limeanza kwenye ukumbi wa Kisota Sekonadri kwa kujadili taarifa za maendeleo ya Kata kwa kila kata inayounda Halmashauri ya Manispaa ya kigamboni ambapo hoja za changamoto ya matundu ya vyoo shule ya Kisota Sekondari na Tungi na ulipwaji wa fidia ya viwanja vya somangila kwa wananchi umetolewa ufafanuzi.
Akizungumza kwa niaba ya Madiwani Mstahiki Meya wa Manipaa ya Kigamboni Mhe.Maabad hoja Amesema kuwa mbali na uchanga wa Manispaa lakini miradi ya maendeleo inaenda vizuri isipokuwa kwa deni la wananchi wa Somangila ambalo limerithiwa kutoka temeke linaendelea kulipwa kwa awamu kadri ya mapato yanavyopatikana.
Kaimu Mkurugenzi Bw.Charles Lawiso amesema kuwa, wananchi wote watalipwa stahiki zao na kwamba malipo yao yaliandaliwa katika mpango wa bajeti changamoto iliyosababisha wasilipwe kwa wakati ni matatizo ya kufungwa kwa mfumo wa fedha ambayo yalijitokeza kwenye ufungaji wa mwaka wa fedha 2018/2019.
Akizungumia changamoto ya vyoo kwa niaba ya Mkurugenzi Kaimu Muhandisi kutoka Manispaa ya Kigamboni Bi. Paskazia Tibalinda amesema kuwa Kisota mkandarasi anamalizia marekebisho ambayo anafanya lakini wakati huohuo vyoo vilivyokamilika Mwalimu mkuu ameandikiwa barua kuanza kutumia vyoo hivyo ili kupunguza changamoto wakati wanasubiri ukamilishwaji wa vyoo vingine.
Aidha ameongeza kuwa wakandarasi wote wa Kisota na Tungi wameandikiwa barua ya kuhakikisha wanakamilisha kazi wanazopaswa kufanya kwa wakati kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kukatwa fedha zao za muda wa uangalizi wa mradi (retention).
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Bw. Abasi Seleman amelipongeza Barazala Madiwani na wataalamu kwa namna ambavyo wamekuwa wakisimamia miradi ya maendeleo , na kushauri kuhakikisha changamoto za vyoo zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati na wananchi wanatatuliwa changamoto zao.
Baraza la Madiwani limeanza leo kwenye ukumbi wa Kisota Sekondari ambapo kesho kutakuwa na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji kutoka kwa Mkurugenzi , taarifa ya Mwaka na uchaguzi wa Naibu Meya na wenyeviti wa Kamati za kudumu.
Kaimu Mkurugenzi Bw. Charles Lawisso akifafanua ulipaji wa fidia kwa wananchi wa Somangila
Wajumbe na wageni waalikwa wakifuatilia Taarifa za Kata zinazowasilishwa na Madiwani.
DIwani wa Kata ya Mjimwema Mhe. Selestine Maufi akitoa hoja ya changamoto ya vyoo Kisota Sekondari leo kwenye baraza.
Baadhi ya Watumishi wakifatilia baraza
Waheshimiwa Madiwani wakifatilia Taarifa za Maendeleo ya Kata ya Somangila
Diwani wa Kata ya Somangila Fransis Masanja akiomba ufafanuzi wa malipo ya wananchi wanaodai fidia ya Viwanja Somangila.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Bw. Abasi Seleman akipongeza Baraza na watendaji kwa kazi wanazofanya.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa