Na. Minde Honorata
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo amewataka wananchi wa Kata ya Somangila kushiriki upatikanaji wa chakula mashuleni.
Hayo ameyasema leo Juni 27,2023 alipokua akihutubia katika kikao cha wananchi mara alipowasili katika mtaa wa Mkwajuni,Visikini, Bamba, Dege na Malimbika iliyopo kata ya Somangiala ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Mtaa kwa mtaa.
Mh Bulembo amesema kila mzazi anawajibu wa kushiriki upatikanaji wa chakula kwa watoto wa shule hasa zile za msingi kwani takwimu zinaonesha shule zinazotoa chakula kwa watoto zina kiwango kikubwa cha ufaulu ukilinganisha na zile ambazo hazitoi chakula.
Aidha Mhe. Bulembo alisema pamoja na Serikali kujikita kwenye uboreshaji wa miundo mbinu ya Elimu kila mwaka bado wananchi wanawajibika moja kwa moja katika shughuli zote ambazo zinaweza kuleta chachu za ukuaji kwa watoto na pia kuongeza kasi ya ufaulu.
"Wazazi wezangu hawa ni watoto wetu tena ni Taifa la kesho tukumbuke kuwa mtoto anajengewa msingi bora wa Elimu kuanzia darasa la awali hadi la saba hivyo tujikite kusimamia elimu ya mtoto huku tukizingatia ulaji wa lishe iliyo bora"
Aidha Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuwa walinzi kwa watoto wao na kujenga utamaduni wa kuhoji mienendo na ratiba zao za kila siku ili kuwasaidia kutambua changamoto wanazokutana nazo na kuzipatia utatuzi kwa haraka.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa