Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo amewataka walezi na wazazi kushirikiana na uongozi wa shule katika kuhakikisha watoto wanapata chakula wanapokuwa shuleni ili kuongeza ufaulu.
DC Bulembo ametoa agizo hilo asubuhi ya leo jumatano ya tarehe 05/07/2023 katika ziara yake katika Kata ya Kibada iliyofanyika kwa lengo la kujitambulisha kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Aidha Dc amepiga marufuku wafanyabiashara wanauza bidhaa zao pembezoni mwa barabara na amewataka kuhamia maeneo rasmi ikiwemo soko jipya la Kibada ambalo limetengenezwa mahususi kwaajili yao
Sambamba na hilo amewataka wamiliki wa viwanja ambavyo havijaendelezwa ndani ya Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha wanavifanyia usafi kwa lengo la kupunguza uhalifu kwani vichaka hivyo vimekuwa vikitumika kama maficho ya wezi na vibaka.
Kwa upande mwingine amepiga marufuku waendesha bodaboda wanaosafirisha nondo na mbao kwa kuziburuza kwenye barabara za lami kwani kunadahifu uimara wa barabara.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa