BODI YA AFYA MANISPAA YA KIGAMBONI YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA AFYA,
Hayo yamejiri leo 2/5/2023 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ambapo Idara ya Afya imekabidhi kwa bodi taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Afya kwa kipindi cha januari-machi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.
Akiwasilisha taarifa hiyo ya utekelezaji Kaimu Mganga Mkuu ndg.Dr.Mohamed Mnyau amesema miradi hiyo ni ujenzi wa jengo la wazazi Zahanati ya Buyuni iliyogharimu kiasi cha shilingi mil.500 zikiwa fedha za ruzuku na mil.12.6 ikiwa ni fedha za mapato vya ndani jengo hili limekamilika na huduma zinatolewa kwa wananchi.Mradi mwingine ni Kituo cha Afya Tundwi Songani unatekelezwa kwa fedha za ruzuku mil.500 na mapato ya ndani mil.81,katika mradi huu tayari huduma zimeanza kutolewa kwa wagonjwa wa nje ambapo upande wa maabara jengo la kujifungulia wazazi yapo katika hatu za za mwisho za umaliziaji.Mradi mwingine ni ujenzi wa jengo la wazazi na upasuaji ,jengo la maabara na jengo la kufulia katika Kituo cha Afya cha Chekeni Mwasonga ambapo mpaka kukamilika kwake kutagharimu shs.mil.450 fedha za ruzuku na mil.70 mapato ya ndani mradi upo katika hatua za umaliziaji.
Aidha ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya Kijaka ni mradi mwingine ambao utekelezaji wake upo katika umaliziaji ambapo upo katika hatua za kupachika mipango kiasi cha fedha ni shs mil 50 za ruzuku na mil.31.3 fedha za mapato ya ndani.
Na miradi mingine ni ujenzi wa jengo la wazazi ,jengo la upasuaji na jengo la kufulia katika Kituo cha Afya Kichangani upo kwenye ukamilishaji utagharimu kiasi cha Shs.mil.500 fedha za serikali kuu na mil.40.1 fedha za mapato ya ndani aidha mradi uliokamilika wa kituo cha Afya Kibada uliogharimu mil.640 mingine ni ujenzi wa wodi 3 hospitali ya Wilaya utakaogharimu mil.500 za serikali kuu na mil.100 mapato ya Manispaa,ujenzi wa jengo la Zahanati Maweni mil.22.4 fedha za mfuko wa Jimbo na mil.49 fedha za Manispaa lipo katika hatua za ukamilishaji , ujenzi wa jengo la MDR (Kifua Kikuu Sugu)Kata ya Vijibweni kiasi cha mil.680 zitatumika hadi kukamilika fedha ni za Global Fund .
Aidha kuhusu tatizo la upungufu wa watumishi katika vituo vya Afya na hospitali Kigamboni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi.Catherin Valence ametaka kujua kutoka kwa Katibu Idara ya Afya bi Digna Zenda mikakati iliyopo ili kukabiliana na tatizo ambapo Katibu huyo Bi.Digna amesema kwamba mikakati ipo ambapo tayari katika Bajeti ya 2023/2024 wameomba Wizara iwapatie watumishi 100 lakini pia wamekuwa wakiwaajiri watumishi kwa mikataba na kuwalipa kwa kutumia mapato ya ndani ili kupunguza tatizo aidha katika ajira zilizotangazwa na TAMISEMI wana tumaini kwamba Kigamboni itapata angalau kiasi flani cha watumishi ili kutatua tatizo,aidha Wizara ilileta watumishi 58 baada ya Manispaa kuomba ambapo watumishi hao wamepelekwa katika vituo vya Afya kuhudumia.
Akihitimisha kikao bi.Catherin amewataka watendaji hao kusimamia miradi inayoendelea kutekelezwa kwa ukaribu na kuhakikisha mafundi hawasababishi dosari katika ujenzi ilibmiradi iweze kuwa na ubora unaotakiwa
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa