Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigamboni limempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu sambamba na ujenzi wa barabara.
Akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichokua na lengo la kupitia taarifa za robo ya kwanza 2023/2024 Meya Manispaa ya kigamboni ambaye ni Diwani wa kata ya Tungi mhe. Ernest Mafimbo amesema takribani kiasi cha zaidi ya bilioni 5 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ndani ya Manispaa hiyo.
Aidha Mhe. Mafimbo amewataka wataalam ngazi ya Wilaya, kata na mitaa kusimamia miradi kwa weledi huku akiwasisitiza kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi kulingana na thamani ya fedha.
" Hatuhitaji usimamizi wa nguvu tunataka yale tuliyoyazimia yafanyike ili kikao kinachofuata tupate taarifa ya utekelezaji kwa kiwango cha hali ya juu. Alisema Mstahiki Meya.
Naye Afisa Mazingira Juvenalis Mauna
anayemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa amesema kwa wilaya ya kigamboni kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tayari wamefikia asilimia 96 ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha Mauna amesema kila kata ndani ya Wilaya ya kigamboni imepewa kiasi cha Tsh Mil. 20 kwa ajili ya uboreshaji wa barabara za mitaa na mpaka kufikia sasa barabara zote zinapitika nyakati zote.
Sambamba na hilo Mauna alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Kigamboni kwa kujitoa na kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa madarasa katika mitaa na kata zao yenye lengo la kuwaletea karibu huduma za kijamii.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa