Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni likiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa Mheshimiwa Stephano Waryoba leo tarehe 16/02/2023 limepitisha makadirio ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yenye jumla ya kiasi cha Tsh Bil 57.3 ambapo kati ya fedha hizo Tsh bil 13.1 ni makusanyo ya ndani, Tsh bil 31.2 ni fedha kwaajili ya mishahara Tsh mil 823.3 ni ruzuku ya matumizi mengineyo Tsh bil 7 ni ruzuku ya miradi ya Maendeleo kutoka Serikali kuu na Tsh bil 3.2 ni fedha kutoka katika mifuko mbalimbali ya Wafadhili
Aidha akiainisha vipaumbele Mheshimiwa Naibu Meya amesema kuwa Manispaa ya kigamboni inategemea kukusanya na kutumia kiasi cha Tsh Bil 16 ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na adhima ya Serikali ya kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia Wananchi.
Sambamba na hilo pia aliwashirikisha baaddhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo Manispaa iliweza kujenga Kituo cha Afya cha kibada kutokana na mapato ya ndani, ujenzi wa Machinjio kupitia mapato ya ndani pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha A fya Tundwi songani
Akiongea wakati wa kikao hicho mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Sikunjema Shabani amesema kuwa bajet ni msingi na ukikoseq kwenye bajeti umekosea mipango yote hivyo Alisisitiza wataalamu kuzingatia vipaumbele muhimu katika kuandaa bajeti
Aidha aliwataka wataalamu kuzingatia maamuzi yanayotolewa na kikao na kuyatekeleza kwa ufanisi kwa lengo la kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa