Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigamboni kwa pamoja limeazimia kupinga kutwaliwa kwa viwanja namba 1-4 kitalu Q na Kamishan wa Ardhi vilivyopo eneo la Vijibweni kwakua Halmashauri ilikuwa imekwisha panga matumizi yake na imeshatumia gharama kubwa kuvipimaa na kwamba vitasaidia kuinua uchumi wa Halmashauri kama chanzo cha mapato.
Azimio hilo limefikiwa mara baada ya Halmashauri kupokea barua kutoka kwa kamishna wa ardhi kuwa eneo hilo limetengwa kuwa benki ya ardhi tofauti na Baraza la Madiwani lililvyoelekeza ambapo utekelezaji wake ulikuwa tayari umekwishaanza.
Akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Maabad Hoja alisema kuwa walitenga eneo ili kuweza kulitumia kwaajili ya kupata fedha ili kuibusti Halmashauri ili ikae sawa na Halmashauri nyingine badala ya kuitwa changa iweze kusimama lakini, bahati mbaya Wizara ya Ardhi imelichukua na kupanga matumizi mengine na kuzia tusisonge mbele.
"tumeshaunda timu ya kwenda wizarani kupambana ili eneo liweze kurudi kwenye Halmashauri yetu kwa manufaa ya Manispaa ya Kigamboni".Alisema Meya
Diwani wa Kata ya Kimbiji Mhe.Sanya Muhidini Bunaya kwa niaba ya madiwani alizungumza kwa masikitiko na kusema kuwa kupitia kamati ya fedha, iliizinishwa fedha ili kuweza kupima eneo hilo ambalo tayari lipo kwenye mpango, sasa haiwezekani kamishana atuandikie eneo hilo kuwa benki ya ardhi na kwamba hatutahusika nalo tena .
"kwanini tuwe tunaingiliwa kwenye maeneo ambayo tayari sisi tumepanga kwa matumizi kwa manufaa ya wanakigamboni wizara inavichukua, sisi leo tunaomba na tunatoa tamko kuwa viwanja hivyo vinne tunamuomba Waziri kupitia kwa katibu mkuu viwanja hivi tunavihitaji kwa matumizi ya Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni" Alisema Bunaya.
Kikao cha Baraza la Madiwani kilifanyika juzi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Kisota.
Kaimu Mkurugenzi Ndg.David Sukali akitoa ufafanuzi wa barua iliyotoka kwa Kamishna wa Ardhi.
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakisikiliza kwa makini kikao cha Baraza
Diwani wa Kata ya Kimbiji Mhe. Sanya Bunaya akitoa masikitiko yake ya kutwaliwa kwa viwanja hivyo
Watumishi wakisikiliza kwenye mkutano wa Baraza
Mastahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Maabad Hoja akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo.
Waheshimiwa Madiwani wakifatilia kikao cha Baraaza.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa