Baraza la madiwani kwa Pamoja leo limeomba wizara ya ardhi kuliachia eneo la tungi (eneo la viwanda) ambalo Manispaa lilijipangia matumizi kwa lengo la kuongeza mapato kwa kutumia wawekezaji baada ya jitihada za awali kutoleta matokeo chanya
Akizungumza kwa niaba ya madiwani mstahiki Meya Mhe. Ernest Mafimbo amesema ni takribani miaka miwili wamekuwa wakifuatlia umiliki wa eneo hilo ambalo lipo ndani ya Manispaa ili kuweza kulitumia kwani kwa sasa eneo lile limeonekana kutokuwa na chochote kinachoendelea zaidi ya kulundikwa takataka.
“ Tumewaelekeza watendaji kurudi tena wizarani ikiwezekana wamfikie hadi Waziri na kuona namna bora ambayo inaweza kufanyika ili lile eneo liweze kuwa miliki halali kwa Manispaa kwani mpango wa matumizi tulionao ni Mzuri na kwakiasi kikubwa umelenga kuongeza Mapato yatakoyotuwezesha kutekeleza miradi yetu ya maendeleo”Alisema Meya
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale akizungumzia mafanikio ya Mwaka wa fedha uliopita na mipango ya mwaka wa fedha ujao amewashukuru Waheshimiwa Madiwani Pamoja na watendaji kwa ujumla kwa namna ambavyo wameweza kushirikiana kwenye suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani katika ukusanyaji mapato kwa kufikia 109%.
Aidha pia ameishukuru sana Serikali kuu kwa kuendelea kuwezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Manispaa kwa kuipatia fedha zaidi ya asilimia 94 ambazo zilielekezwa kwenye sekta ya elimu, ambapo kwenye elimu bila malipo Elimu Msingi Mil.400 , Elimu sekondari zaidi ya Bil.1, Sekta ya afya kwa kuongeza ujenzi wa wodi 3 Hospitalini milion 500, milioni 150 kwaajili ya kuendeleza Zahanati na ujenzi wa vituo vya afya 2 vya tundwi songani milioni 400 Pamoja na chekeni mwasonga milioni 500.
Ameongeza kuwa Sekta ya elimu imekuwa na changamoto kubwa sababu ya ongezeko la wanafunzi kutokana na elimu bila malipo kama ambavyo taarifa ilivyoonesha hivyo tumejipanga kuhakikisha tunaboresha miundombinu kwa kutenga Milioni 800 kutoka mapato ya ndani kwa elimu Msingi na Sekondari ambalo pia ni agizo la Serikali kupitia TAMISEMI.
Kwa upande wa Miundombinu ya barabara na mitaro amesema imekuwa ni changamoto nyingine kubwa kwani kwa awamu zilizopita Kigamboni haikuweza kuwekwa kwenye miradi ya DMDP na ilibaki nyuma sana sababu ya ule mpango wa KDA ambao haukuruhusu uendelezaji Hivyo kama Manispaa imeweka bajeta ndogo kwa kuanzia kama Mil 144 ambazo zitaelekezwa kwenye kusaidia na itaendelea kuongezwa kadri ya mapato yatakavyokuwa yanaongezeka.
Mkutano wa Baraza wa kufunga mwaka wa fedha 2020/2021 limefanyika leo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kigamboni.
Mkurugenzi wa Manispaa Erasto Kiwale akielezea mafanikio na mikakati ya utekelezaji wa miradi kwa mwaka wa fedha 2020/2021
Waheshimiwa Madiwani wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya kufunga mwaka wa fedha 2020/2021
Wataalamu wa Manispaa wakifatilia uwasilishwaji wa taarifa kwa makini kwenye ukumbi wa Manispaa Leo.
Diwani wa kata ya Kibada akichangia mada Mara baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya kufunga mwaka wa fedha 2020/2021
Wataalamu wa Manispaa wakifatilia uwasilishwaji wa taarifa.
Diwani wa Kata ya Kigamboni Mhe.Dotto Msawa akiwasilisha maeleekezo ya kurudi tena Wizarani na kuomba umiliki wa eneo la Tungi (Viwandani)
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa